Kama unataka kua mfanya biashara mkubwa kua hivi

Katika sayari hii idadi kubwa ya shughuli ambazo hufanywa na mwanadamu ni biashara, kama ndivyo hivyo basi naomba niweze kujikita zaidi katika kulizungumzia jambo hilo siku ya leo. Na siku ya leo nataka kusema jambo moja ambalo kila mfanyabishara anapaswa kulifahamu ili kujikuza katika biashara yake. Na jambo hilo wafanyabiashara walio wengi wamekuwa wakilitumia kinyume chake hata kupelekea wao wenyewe kutokufanya vizuri katika tasnia ya biashara. Wengi wa wafanyabiashara wanafikiria kufanya hivyo ni kukua kibiashara kumbe si kweli. Japo hilo si lingine bali kusema uongo juu ya biashara ambazo wanazifanya. Jambo hili limekuwa likiwafanya wateja wengi kuhama na kwenda sehemu zingine, na kitendo hicho hufanya mfanyabiashara kupoteza wateja bila ya yeye mwenyewe kujijua. Na kutoka na uongo ambao wanautumia wafanyabiashara wengi wamekuwa , vinara wa kulalama ya kwamba vyuma vimekaza, huku wao wenyewe ndio chanzo cha kukuza kwa vyuma hivyo...