NJIA TATU BORA ZA KUUWA USHINDANI KATIKA BIASHARA YAKO


Ushindani imekuwa moja kati ya changamoto kubwa sana miongoni mwa wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara kutokana na kuwa siku hizi watu wengi sana wamekosa ubunifu kwa kile wanachokifanya. Sasa hivi ukianzisha biashara mpya tu baada ya muda unakuta jirani yako ameshakuiga tayari na mnaanza kugawana wateja na swala la wateja linaanza kuwa gumu na unashindwa kuuza bidhaa au kutoa huduma uliyokusudia kwa wateja wako husika. Ila usiwe na shaka njia hizi tatu zitakusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupunguza au kumaliza kabisa ushindani sokoni.
1.Elewa mteja wako ni nani.
Jambo hili ni muhimu sana miongoni mwa wajasiriamali kwani humfanya mjasiriamali kujua hasa ni kitu gani mteja wake anahitaji na wakati gani ampatie kama ni bidhaa au huduma anayotoa kwa ubora wa hali ya juu, na ukishaelewa mteja wako ni wa aina gani inakuwa rahisi sana kwa wewe kuuza kwa sababu utajua ni kitu gani au ni vitu gani anavipendelea zaidi kutoka kwako na wewe utaongeza juhudi zaid kumpatia ili kusudi aendelee kuja kwako kila siku.
Ukishaelewa mteja wako ni nani utakuwa tayari umejitofautisha na wengine wengi kwani wafanyabiashara wengi au hata wajasiriamali hawajui kuwa wateja wao ni kina nani, na kama hawajui maana yake wahaelewi wateja wao kuwa ni kitu gani wanapenda na kitu gani hawapendi sasa kwanini usimpoteze huyo mteja ? lazima apotee amini usiamini.
2.Kuwa mtaalam/special  kwa jambo unalolifanya.
Hakikisha unakuwa mtaalam kwa kile kitu ufanyacho iwe ni biashara ya kutoa bidhaa au huduma Fulani, hakikisha unautaalam wa kipekee ambao haufanani na mtu mwingine. Tatizo lilipo miongoni mwa wajasiriamali wengi ni kuwa wanataka wafanye kila kitu kwa wakati mmoja Mfano unakuta mtu kafungua duka la kawaida hapo hapo anaweka kibanda cha kuuza nyanya au vitu mbalimbali na asubuhi unamkuta mtu huyo huyo anauza vitumbua ikifika jioni anamkuta na shughuli nyingine. Sasa kwa hali hii ya kufanya kila kitu utakuwa mtaalam au special  kivipi kama unafanya kila kitu?.Ili uwe special lazima utazame jambo moja na ulifanye kwa ubunifu wa hali ya juu na wa kipekee na watu wakakufahamu kwa jambo hilo tu moja, lazima uondoe ushindani sokoni na hata kama watu watakuiga hawataweza kufanya kama unavyolifanya wewe.
3.Tengeneza brand yako kwa wateja wako.
Ili uweze kunielewa hapa ngoja nikupe Mfano mtaa ninaoishi mimi kuna mafundi cherehani wengi sana ila miongoni mwahao mafundi cherehani kuna mmoja wao anasifika sana kwa kushona nguo kwa wakati yaani kama umepeleka nguo yako leo na akakuambia njoo uichukue kesho asubuhi basi jua kuwa ikifika wakati huo utaikuta nguo yako iko tayari lakini sio kweli kuwa ushonaji wa fundi huyu ni bora sana kuliko hawa wengine, ila tu yeye anasifika kwa kuwa mkweli na muaminifu ukimpa kazi yako anaifanya kwa wakati muafaka mliokubaliana, na anapata wateja wengi sana kuliko hawa wengine na sababu ni moja tu ametengeneza brand yake ya kipekee kwa wateja wake Hivyo hana ushindani kwa kile anachokifanya.
Mpaka hapa umeona umuhimu wa kutengeneza brand yako usifanye biashara kwa mazoea itakufa tu amini usiamini huu ndio ukweli tengeneza brand yako kwa kile unachokifanya hata kama unauza miogo au unapika chapatti hakikisha unakuwa na sifa ya kipekee kabisa kwenye soko utafanya biashara kwa furaha sana bila kuwa na ushindani wowote.
Haya ndio mambo makuu matatu ya msingi unayotakiwa wewe kuwa nayo kama mjasiriamali unayetaka kuwa ushindani ndani ya soko kwa kile unachokifanya, natumaini umependa mafunzo haya mazuri sana kwako jaribu haya kwenye biashara yako utapata matokeo makubwa sana. NAOMBA SUPPORT YAKO KWA KUIPA NYOTA TANO APP HII PLAYSTORE ILI IWEZE KUFIKIA WATU WENGI ZAIDI NA WAO WANUFAIKE NA MAFUNZO HAYA. ASANTE

Comments

Popular posts from this blog

Njia 7 za kukuingizia hela hata kama umelala

Kilimo bora cha chainese

Siri tano za mafanikio bila kua tegemezi