Jifunze saikolojia ya biashara kupata mafanikio haraka

Unaijua saikolojia ya biashara? Unajua tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo binadamu tunalo ambalo linapelekea kutofanikiwa katika biashara zetu? Unajua msigano wa yaingiayo ndani yetu na yale tuyaaminiyo ni ugonjwa mkubwa sana wa kisaikolojia ambao kila mtu anatakiwa kuutibu?
Saikolojia ya biashara ninini?
Kwa lugha nyepesi ni saikolojia inayojikita kuhakikisha wafanya biashara wananufaika na biashara zao. Hili hufikiwa kwa kuhakikisha mahusiano bora huwepo kati ya mtu na mtu na kati ya biashara na biashara.
Mambo gani ya kujifunza?
Jambo kubwa la kujifunza ni kuwa na fikra chanya muda wote. Unapoambiwa jambo ambalo linakinzana na unachoamini usilipokee kwa mtazamo hasi.
Kwa mfano
Mmetofautiana lugha na mteja ama msaidizi wa kazi zako usipeleke fikra zako upande hasi bali zipeleke upande chanya. Hebu waza kwanza je ni mara ngapi amelifanya jambo hilo? Kama ni mara ya kwanza basi jipe tumaini kuwa ni bahati mbaya tu. Kama ni mara nyingi basi usimlaumu yeye bali muonee huruma mana hajui alitendalo.
Inaaminika kuwa binadamu wa kawaida ni nadra sana kufanya jambo kwa minajili ya kumuona mwingine akikasirika. Kinachotokea na kumkasirisha mtu bila kukusudia.
Katika biashara utakwazwa na mengi sana. Hata kupata shoti hukwaza sana. Bali ukiwa na fikra chanya basi utaamini kila litokealo lina mlango wa kutokea.
Miongoni mwa masuala yapewayo kipaumbele
Kujifunza saikolojia ya biashara kunajumuisha kupitia makala kadhaa zihusuzo:
  1. Namna ya kuchagua mwenza katika biashara,
  2. Namna ya kuchagua wafanyakazi,
  3. Namna ya kutathmini wafanyakazi,
  4. Kuwafunza wafanyakazi mbinu za kuongeza uzalishaji,
  5. Kujifunza na kuwafunza wafanyakazi uongozi,
  6. Kuibua na kuendeleza vipaji,
  7. Mazingira salama na rafiki ya kazi,
  8. Kuboresha utamaduni wa kupendana na kuhurumiana,
  9. Kuboresha utamaduni wa kushikiana, etc etc
Hitimisho
Kupokea ushauri na kusoma sana masomo ya namna ya kudhibiti hasira, mihemko, jazba, ukakasi, etc etc ni sehemu muhimu sana katika hatua za kuboreaha saikolojia yako ya biashara. Kujifunza mahusiano na mawasiliano chanya pia hupelekea kujinoa kuelekea kwenye mafanikio ya kuboreaha saikolojia yako ya biashara.

Comments

Popular posts from this blog

Njia 7 za kukuingizia hela hata kama umelala

Kilimo bora cha chainese

HATUA TANO ZA KUCHUKUA ILI UWE TAJIRI