Jinsi ya kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii

Kama unataka kufanikiwa kukuza biashara kupitia social media (mitandao ya kijamii) basi fuata haya. Katika makala hii ntatumia mfano wa saluni ya urembo inayotaka kukua kuwa kampuni kubwa ya urembo. Mmiliki wa saluni hiyo ana malengo matatu (1) Kukuza saluni yake mpaka ifikie hatua ya kuzaa saluni nyengine sehemu mbalimbali. (2) Afungue chuo cha urembo miaka ya baadae. (3) Kuzalisha bidhaa za urembo ikiwemo manukato, lotion, mafuta ya nywele na kadhalika miaka ya baadae.
Pia ntachukulia kuwa mmiliki wa saluni anajua kuwa hayo hapo juu hayawezi kuitwa malengo mpaka yakidhi vigezo vya kuitwa malengo. Kabla hayajakidhi kuitwa malengo huitwa ndoto.
1. Watambue walengwa wako mahususi.
Wazungu huita target customers. Ni watu wa aina gani unalenga kuwauzia bidhaa zako ama ni watu wa aina gani ungependa kuwahudumia? Tuchukulie kuwa mmiliki wa saluni tunayoiongelea ana malengo ya kuhudumia:
=> Wanawake wenye umri wa miaka 20-45.
=> Wanaopenda urembo na umaridadi.
=> Wenye kipato zaidi ya Tshs 350k kwa mwezi.
=> Wanaoishi mijini na jirani na mijini.
2. Chagua mitandao miwili ama mitatu ya kijamii ya kuitumia.
Usihangaike kutaka kuwepo kwenye kila mtandao wa kijamii. Badala yake chagua mitandao miwili ama mitatu na ujikite huko. Takwimu za 2015 zinaonesha kuwa jumla ya watanzania 2.8m hutumia fb, 610k hutumia insta, 411k hutumia linkedin, 168k hutumia twitter. Takwimu hizo hizo zilionesha kuwa kila mtumiaji wa youtube huangalia video takriban mara 11. Tuchukulie kuwa tumeamua saluni yetu iwe na ukurasa wa fcbk, insta na twitter. Jina la saluni yetu tuchukulie ni MiaMia Fashion and Beauty. Hivyo basi tutatengeneza kurasa hizi:
3. Anza kupost makala
Hapa ndio ambapo wengi wetu hatujui nini cha kupost. Watu wengi waliopo mitandaoni huwa hawapendi matangazo. Wengi wetu tukikutana na matangazo mitandaoni tunaruka na kwenda kusoma jambo jengine. Hivyo basi usije ukaanza kutangaza bidhaa zako badala yake elezea matatizo ambayo walengwa wako mahususi wanakumbana nayo na namna ya kuyatatua. Mfano kwa saluni inayotamani kuwa kampuni ya urembo inaweza kuwa inapost matatizo yanayohusu sababu na suluhisho la kukatika katika kwa nywele, kufubaa kwa ngozi na suluhu, masuala ya kuungua na cream na namna ya kujiepusha na suluhu, mazoezi muhimu ili mtu awe na shepu yenye mvuto milele, na kadhalika na kadhalika.
Hapa ndio sehemu ya kuonesha picha mbalimbali za aina ya misuko uliyokwisha wasuka wateja wako. Usikopi picha ilimradi zipo mitandaoni ukaziweka tu. Lazima ujue kuwa watu wanapenda kitu live sio kilichonakiliwa.
Unaweza weka video za matukio ya ususi na urembo. Ita kamera man wanaotumikaga kwenye maharusi. Mwambie atoe vipande vizuri vya video kadhaa. Weka kwenye kurasa hizo za fbk na insta.
Ila kumbuka yote kwa yote lazima wewe mwenyewe kila mwaka usome japo kozi moja fupi ya masuala ya urembo. Fanyia majaribio kila unachokisoma. Endapo unataka saluni yako ikue na iweze kufikia kuwa na brand yake ya nywele, vipodozi, manukato na kadhalika basi lazima ujitolee muda mwingi sana kusimamiasaluni yako. Wewe mwenyewe ndio unapaswa ujue fashion nyingi zaidi ya wale ulowaajiri.
Kadri unavyofundisha mitandaoni mambo ya urembo ndivyo utavyoona uhitaji wa kufungua shule ya urembo unavyojitokeza. Ikifikia huko basi anza taratibu kwa kukodi ofisi kubwa zaidi ya kurembea watu na kufundishia pia.
4. Busti makala zako ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi
Unapobusti makala kwenye mitandao ya kijamii makala zako zinawafikia watu wengi zaidi na hatimae unakuwa maarufu ndani ya muda mfupi. Kwa kawaida napendekeza utumie dola 1 kila siku kwa ajili ya kugaramia ukurasa wako wa fcbk na dola moja kila siku kugaramia ukurasa wako wa insta. Hii itakusaidia kubusti makala moja kila siku ama kubusti makala kwa zaidi ya siku moja.
Katika hili nashauri uwekeze japo shilingi 5,000 kila siku ya ziada umlipe mtu ambae anajua kutengeneza makala zenye mvuto na kuzilipia anapozibusti ili isiwe tabu kwenye masuala ya kulipia kwa kutumia kadi za kielektroniki. Unajua mtu anaefanya hii biashara ya kuwatengenezea watu brand kupitia mitandaoni anakuwa ana wateja wengi kwaiyo analipa mara moja ama mbili kwa mwezi kwa ajili ya wateja wake. Inampunguzia makato. Mfano rahisi ni kama mpesa ama tigo pesa inavyokata kwa kila muamala unaoufanya. Pia kutumia mtu mjuzi wa kutangaza kupitia mitandao ya kijamii itakusaidia kujua namna ya kuchagua walengwa mahususi ili kila makala inayobustiwa inaonekana na wale tu ambao tunaamini kwa namna moja ama nyengine wanaweza kuwa wateja wetu kulingana na mkoa walipo, umri wao, kipato chao na kadhalika.
5. Sio mbaya kutenga bajeti pole pole ya kununua simu inayotoa picha nzuri
Hii itasaidia wewe kupiga picha nzuri sehemu tofauti tofauti zihusuzo urembo na masuala anuwai ya kijamii na kupata picha za kuweka kwenye kurasa zako za fcbk na insta.
Nakuhakikishia ukifuata utaratibu huo hapo juu saluni yako itajulikana na kila mtu alie kwenye rika la walengwa wako mahususi na itakuwa na wateja wengi na utapata pesa ya kupanua wigo wa biashara. Ila usisahau kusoma kozi mpya kila mwaka. Kubali kipato kidogo kwa kuwekeza asilimia kubwa kujielimisha na kujenga jina la biashara mwanzoni ila ndani ya miaka miwili utakuwa mtu wa tofauti sana.

Comments

Popular posts from this blog

Njia 7 za kukuingizia hela hata kama umelala

Kilimo bora cha chainese

HATUA TANO ZA KUCHUKUA ILI UWE TAJIRI