Kua mjasiriamali kwa kufuga kuku wa asili
Mwanza: Ujasiliamali ni moja ya hatua katika mapambano dhidi ya umasikini, lakini pia ili kuweza kuwa mjasiriamali, yanahitajika maarifa ya ziada, ikiwamo ubunifu katika kuboresha shughuli unazozifanya ili ziwe na tija.
Kama unaamini kweli kuwa unataka kuanzisha biashara yako mwenyewe lakini hujapata wazo la biashara lililostahiki, pumzika kwanza, halafu baada ya wiki moja au zaidi anza tena kuangalia mawazo mengine ya biashara kupitia Makala hii.

Leo hii nitawaelezea kuhusu biashara ya kufuga kuku wa kienyeji ambavyo inaweza kukukwamua kutoka kwenye umasikini kwa kuwawezesha watu kutengeneza ajira zao binafsi.
Nilipomtembelea mfugaji mwenye mafanikio jijini hapa, Bazil Dotto Bazil, nyumbani kwake Mh’andu Jijini hapa, ambapo alinisimulia kilichomsukuma kuingia katika ujasiriamali wa kufuga kuku wa kienyeji.
“Watu wengi katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Technolojia wamekuwa wakiathirika na magonjwa mbalimbali kutokana na ulaji mbaya wa vyakula vyenye madawa hususani Kuku wa kukuza kwa madawa, hata hivyo Madaktari wamekuwa wakiwashauri watu kula kuku wa kienyeji ili kulinda Afya zao, ndipo nikapata wazo la kuanza kufuga kuku hawa mwaka 2012” alisema Bazil.

“Nilianza kufuga kuku Mei 10, mwaka 2012 baada ya kuibuka mshindi katika shindano la fanikiwa kibiashara (BDG) na kupatiwa sh4.4mil, nikaanzia vifaranga 100 ambao kila kifaranga nilikinunua sh600 sawa na sh600, 000 ambao nimekuwa nikiwauza bila kuongeza kutokana na mtaji kuwa mdogo japokuwa nilipata faida ya sh500, 000, kutokana na fedha nyingine kununulia mashine ndogo ya Incubator ambayo haikunisaidia sana ndiyo maana sasa nimenunua hii kubwa yenye thamani ya sh700, 000” alisema Bazil.
Akielezea aina ya kuku anaowafuga, alisema amekuwa akifuatilia aina mbalimbali za kuku wa kienyeji na akaridhia kufuga aina moja iitwayo kuchi, hao ni jamii ya kuku wanaofugwa katika mikoa ya kanda ya kati na Ziwa Victoria wenye umbile kubwa na nyama tamu inayopendwa na watu wengi ambao anaamini kuwa kwa kutumia mashine hii atapata fursa ya kuzalisha vifaranga vingi kwa wakati mmoja.
“Kuku wa kienyeji hutaga mayai madogo yenye uzito wa gram 28 hadi 42, ambapo kuku wa kigeni hutaga mayai makubwa kati ya gramu 56 hadi 70; huanza kutaga wakati amefikia kwenye umri wa majuma 20, wanafikia uzito wa kilo moja na robo wakati wana umri wa majuma 21, ambapo baadhi ya kuku wa kigeni wanaweza kufikia uzito wa kilo moja na nusu kati ya majuma 8 hadi 12” alisema Bazil.
“Kama kuku akitunzwa vizuri kutokana na mbinu bora za ufugaji, anaweza Kuongeza uwezo wa kutaga mayai kutoka mayai 10 hadi mayai 12 kwa mwezi, ambapo kwa kutumia mashine hii naweza kuweka treyi kumi kwa muda wa siku 21 kwa mayai yaliyotangwa ndani ya siku tatu hadi kumi na mbili huku nikizingatia kuyageuza mara tatu kwa siku, baada ya siku 21 nitakuwa na vifaranga 300 ambavyo nitakuwa na uhakika wa kuwakuza wote; Kwa mfano ukiwa na kuku 12 na jogoo mmoja waliolishwa kilo moja ya nafaka kila siku unaweza kuuza treyi 10 za mayai kila mwezi ambayo ni sawa na mayai 4 kila siku, huku treyi moja ikiuzwa kwa sh15,000” anasema Bazil.
Akitoa mfano wa mchanganuo wa mahesabu ya ufugaji Kwa kipindi cha miaka miwili.
Akitoa mfano wa mchanganuo wa mahesabu ya ufugaji Kwa kipindi cha miaka miwili.
Bazil alisema kuwa, Kwa mtaji wa Sh500, 000 kama una eneo la ekari moja na mabanda ya kutosha kiasi cha kuku 10,000. Ukianza kwa kufuga kuku 25 (kuku jike 20 na jogoo watano) ambao utawanunua kwa Sh250, 000. Hao kuku 20 wakianza kutaga vifaranga 10 kila mmoja, wataangua vifaranga 200 watunze vizuri katika vifaranga hao tuchukulie majike yanaweza kuwa 150 ambao ndani ya miezi sita au zaidi nao wataanza kutaga; Kipindi hicho utakuwa na kuku (200+ 25 =225.) Baada ya hiyo miezi sita kuku watakaotaga ni 170 kila mmoja akipata vifaranga 10 mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku (1700+20+55=1775) ukiuza kuku 1,000 kwa bei ya Sh10, 000 utapata Sh10, 000,000.
Na kuongeza, Mwaka wa pili majike 775 yakiangua vifaranga 10 kila mmoja, utakuwa na kuku 7,550 mwisho wa mwaka ukiuza kuku 3,000 kwa bei ya Sh10, 000 utapata Shs. 30,000,000; Hesabu hizi ni kwa makadirio ya chini sana kwani kama nilivyoelezea hapo juu kuku mmoja kama atatunzwa vizuri anaweza kuataga mayai kati ya 10 hadi 12 kwa mwezi na unaweza pia kuuza mayai, huku treyi moja ikiuzwa Sh15, 000 sawa na mayai 30.
Anafafanua kuwa, ufugaji wa kuku wa kienyeji una changamoto kubwa hasa kwa upande wa gharama za chakula ambapo upatikanaji wa pumba umekuwa adimu kutokana na watu wengi kula wali kutokana na kushuka kwa bei na kupelekea gunia kuuzwa kwa sh20, 000 kutoka sh12, 000 ya awali, huku katika kipindi cha mwezi wa Juni, hadi Oktoba, dagaa hupanda bei na Ziwa Victoria ni pekee linalotoa dagaa wengi katika nchi za Afrika mashariki na kati, hivyo kushindwa kutosheleza mahitaji ya walaji na kusababisha sisi wafugaji kununua bei ya juu, umeme si wa uhakika.

“Ni muhimu kuzuia na kutibu magonjwa kwa mujibu wa kutokea kwa magonjwa,kwani chanjo huenda ikawaua ndege ambayo tayari ni wagonjwa.Kupanga utoaji wa chanjo na matibabu,unashauriwa kutumia inayoitwa‘kalenda ya kuzuuia magonjwa’,ambapo madaktari wa wanyama,wakulima na wafanyakazi wa nje wanaweza kutambua vipindi ambavyo magonjwa yanafaa kuzuiwa ama kutibiwa, Kinachotakiwa kuzingatiwa ni kuwapa chanjo kwa wakati husika, kama vile ‘malex’, ‘new casstle’ ‘Gombollo’ na nyinginezo, vinginevyo ufugaji unaweza kuwa sekta isiyowezekana” aliongeza.
Kabla ya kuanza ufugaji huu, Bazil alisema kuwa, aliwahi kufuga kuku wa kisasa wa nyama mwaka 2003 ambapo alianza na kuku 200 kutokana na kutojua kanuni za ufugaji walikufa 180, na mwaka 2010 pia alifuga kuku wa kisasa wa mayai ambao walikuwa 300 hadi wakafika 400, ila aliacha baada ya kushindwa gharama za uendeshaji kutokana na soko kutekwa na Wakenya na Waganda.
Kwa upande wake muuzaji wa kuku soko kuu, Charles Mgaya aliyeanza kufanya biashara hii, takribani miaka 30 alisema kuwa, changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni ukosefu wa soko kwani kuku wa kienyeji akikaa zaidi ya siku tatu anadhoofika na kuugua, hivyo kushusha bei hali inayopelekea kupata hasara.
“Kuku wa kienyeji tunawanunua kwa kutathimini kwa mfano kuku 50 tunawanunua kwa sh7, 000 kila mmoja lakini tunawauza katika makundi matatu, wakubwa sh8, 000 hadi 12,000, wa kati sh7, 000 na wadogo sh6, 000, gharama inapanda kutokana na usafirishaji kutoka kijijini kuleta sokoni kwa bajaji sh10, 000 na kwa gari sh20, 000, huku chakula kikigharimu sh20, 000 kwa muda watakao kaa hapo” alisema Mgaya.
Na kuongeza kuwa, biashara yenyewe wanafanya kwa mkopo maana wafanyabiashara wengi wanaendesha biashara zao kwa mikopo, huku soko kubwa likitekwa na KUKU POA.

Charles Mgaya ana familia ya watu 12 inayo mtegemea kutokana na biashara ya kuku, huku sita kati yao wanasoma akiwali[pia sh900,000 kwa mwaka; moja ya mafanikio anayojivunia ni kupata nyumba ya kuishi yenye thamani ya sh25mil ila anasema biashara hiyo ilikuwa inalipa miaka ya nyuma kwa alikuwa anaweza kuuza kuku 300 kati ya 400 alionao kwa thamani ya sh300,000 kila mmoja sh300 au 400 fedha taslim, lakini sasa wanauza kuku 30 hadi 40 kwa mali kauli (mkopo).
Nikataka kufahamu kwanini wanapandisha bei siku za sikukuu?
“Sikukuu bei ya kuku inapanda kutokana na madalali kuingilia biashara hiyo, hivyo kuku kutoka kijijini hadi soko kuu anakuwa amepitia mikono mingi na bei tofauti na kwa kuwa wewe unataka kuuza inabidi ununue halafu uuze kwa bei ya juu” alijibu Mgaya.
Kuku wa kienyeji wamekuwa wakifugwa kwa wingi vijijini kwa malengo ya kupata nyama na mayai kwa ajili ya familia husika na kwa ajili ya kupata pesa za kujikimu. Kuku na mayai ya kienyeji yana faida kubwa kiafya kutofautisha na kuku wakisasa ambao hukuzwa kwa kemikali. Idadiya kuku Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya kuku Milioni 34 wanaofugwa na takribani 60.5% ya kaya zinazojishughulisha na kilimo.

Hata hivyo uzalishaji wake umebaki kuwa duni kutokana na changamoto za wafugaji zifuatazo; Utunzaji duni, Udhibiti mdogo wa magonjwa, lishe duni, makazi duni, Uzaliano wa karibu, Teknolojia duni, Kukosekana kwa mtazamo/mwamko wa kibiashara.
Faida ya kufuga kuku wa kienyeji.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji una manufaa mengi kwa mfano; Kuku hutumia eneo dogo kuliko wanyama wengine wa kufugwa, pia hutumia chakula kidogo hivyo ufugaji unaweza kuendeshwa bila kutumia mtaji mkubwa, kwa mfano bei ya nyama kwa kilo moja ni sh3,500 hadi 4,000, huku kuku mwenye uzito sawa uuzwa sh10,000 hadi 18,000.
Kuku wanaweza kupewa mabaki ya chakula pamoja na vyakula vya kujitafutia kama vile wadudu,mbegu na majani; Kazi za usimamizi wa kuku zinaweza kufanywa na mama na watoto.

Kuku na mayai humpatia mfugaji chakula bora na kumuongezea mapato, Pia mfugaji ni kama mtu aliyewekeza fedha zake benki au kwenye kitega uchumi kingine ambapo kuku huweza kuongezeka kutokana na kuku kutaga na kuangua vifaranga kama faida inavoongezeka benki na kwenye vitega uchumi vingine. Mfugaji ni sawa na mtu aliyeweka akiba benki kwani akipata shida anaweza kuuza kuku na kulipa ada, mahari matibabu ya hospitali pamoja na shida zingine.
Kuku wa kienyeji anasaidia kusafisha mazingira kwa kula wadudu na kuongeza rutuba kwa mbolea inayotokana na kinyesi cha kuku ambacho hakina kemikali. Mbolea hii ni nzuri sana na kama inazalishwa kwa wingi inaweza kuwa chanzo kingine cha mapato kwa mfugaji wa kuku.
Kuwa mjasiriamali kwa kufuga Kuku wa kienyeji ana uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa, hutaga mayai na kutunza vifaranga badala ya kutumia mashine, pia anaweza kuishi sehemu yoyote au nchi yoyote duniani bila kuathiriwa na hali ya hewa.

Comments
Post a Comment