Njia rahisi ya kuijua fursa
Kutafuta fursa na kubaini fursa ni zoezi linalowashinda vijana wengi. Fursa ina kanuni tatu rahisi. Zaweza kuwepo nyengine ila hizi ndio kuu. Kanuni hizi zinahusiana na uhitaji, upatikanaji, ubora, huduma.
1. Uhitaji wa bidhaa > Upatikanaji wake.
2. Ubora unaohitajika > Ubora unaopatikana.
3. Huduma inayohitajika > Huduma inayopatikana.
Kama hukumbuki alama hizi acha nikukumbushe.
> kubwa kuliko
< ndogo kuliko
Hivyo basi siku zote angalia soko kwa kanuni hizi tatu. Na ukifuata kanuni hizi utaziona fursa nyingi sana. Hutohangaika kuiga biashara za watu kama hakuna uhitaji wa ziada ama kama ubora upatikanao sio hafifu. Short and clear.
Comments
Post a Comment