Posts

Showing posts from September, 2018

Kama unataka kua mfanya biashara mkubwa kua hivi

Image
Katika sayari hii  idadi kubwa ya shughuli ambazo hufanywa na mwanadamu ni biashara, kama ndivyo hivyo basi naomba niweze kujikita zaidi katika kulizungumzia jambo hilo siku ya leo. Na siku ya leo nataka kusema jambo moja ambalo kila mfanyabishara anapaswa kulifahamu ili kujikuza katika biashara yake. Na jambo hilo  wafanyabiashara walio wengi wamekuwa wakilitumia kinyume chake hata kupelekea wao wenyewe kutokufanya vizuri katika tasnia ya biashara. Wengi wa wafanyabiashara wanafikiria kufanya hivyo ni kukua kibiashara kumbe si kweli. Japo hilo si lingine bali  kusema uongo juu ya biashara ambazo wanazifanya. Jambo hili limekuwa likiwafanya wateja wengi kuhama na kwenda sehemu zingine, na kitendo hicho  hufanya mfanyabiashara kupoteza wateja bila ya yeye mwenyewe kujijua. Na kutoka na uongo ambao wanautumia wafanyabiashara wengi wamekuwa , vinara wa kulalama ya kwamba vyuma vimekaza, huku wao wenyewe ndio chanzo cha kukuza kwa vyuma hivyo...

Funguo tano za mjasiriamali

Image
Kitu kizuri kwa mjasiaramali yoyote yule uwe unaanza au tayari safari hiyo ulishaanza ni kujiandaa kuwa mshindi. Ni muhimu sana kujua wewe ni mshindi kwa kile unachokifanya bila kujali ni changamoto zipi unakutana nazo. Lakini hata hivyo huwezi kuwa mshindi kama hutaweza kujua siri ya ushindi huo utaupata vipi. Kutokana na hilo sasa hapo ndipo unalazimika kuzijua funguo tano za  mafanikio ukiwa kama mjasiriamali. Hizi ni funguo tano kweli kwa mjasiriamali ambazo ukizitumia, zitakupa mafanikio na kukufikisha kule unakotaka kufika . Funguo hizo ni zipi, fuatana nasi katika makala yetu ya leo kujifunza. Weka kushindwa nyuma kabisa. Kwa kawaida huwa yapo makosa  na kushindwa kwingi hasa pale unapoanza biashara au hata pia unapokuwa unaendelea na biashara yako. Yote hayo yanapotokea ikiwa kweli wewe ni mjasiriamali uliyenuia hebu yasahau. Kitu kukubwa kwako angalia kule unakokwenda. Makosa ni sehemu pia ya kukusaidia kufanikiwa kule unakokwenda ikiwa utajifunza. ...

NJIA TATU BORA ZA KUUWA USHINDANI KATIKA BIASHARA YAKO

Image
Ushindani imekuwa moja kati ya changamoto kubwa sana miongoni mwa wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara kutokana na kuwa siku hizi watu wengi sana wamekosa ubunifu kwa kile wanachokifanya. Sasa hivi ukianzisha biashara mpya tu baada ya muda unakuta jirani yako ameshakuiga tayari na mnaanza kugawana wateja na swala la wateja linaanza kuwa gumu na unashindwa kuuza bidhaa au kutoa huduma uliyokusudia kwa wateja wako husika. Ila usiwe na shaka njia hizi tatu zitakusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupunguza au kumaliza kabisa ushindani sokoni. 1.Elewa mteja wako ni nani. Jambo hili ni muhimu sana miongoni mwa wajasiriamali kwani humfanya mjasiriamali kujua hasa ni kitu gani mteja wake anahitaji na wakati gani ampatie kama ni bidhaa au huduma anayotoa kwa ubora wa hali ya juu, na ukishaelewa mteja wako ni wa aina gani inakuwa rahisi sana kwa wewe kuuza kwa sababu utajua ni kitu gani au ni vitu gani anavipendelea zaidi kutoka kwako na wewe utaongeza juhudi zaid kumpatia ili kusudi a...

JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA HATA YA KUWA NA MTAJI

Image
Kwa ufupi Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi ukiwa upande wa huduma na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine na kadhalika. Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndiyo uanzishe biashara na ndiyo sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha. Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu katika kuanzisha biashara, lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa. Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi ukiwa upande wa huduma na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine na kadhalika. Ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi fulani hivi ili uweze kufika kilele cha mafanikio. Hapa simaanishi lazima uwe ...

HATUA TANO ZA KUCHUKUA ILI UWE TAJIRI

Image
Hivi umeshawahi kujiuliza kuwa  ipo siku unaweza ukawa na mafanikio makubwa hadi kufikia utajiri? Kama bado hujawahi kuwaza hivi hata siku moja, leo nataka nikupe habari njema kuwa hata wewe unaweza ukawa tajiri leo hii endapo utaamua. Unashangaa! Ndiyo unaweza. Kwa nini nakwambia unaweza? Sikiliza. Kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri si bahati wala muujiza kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiri sana.  Bali ili uweze kuwa tajiri unahitaji kuwa na maandalizi yakutosha na kuchukua hatua muhimu za kukufikisha huko. Ikiwa utakubali kufanyia kazi hatua hizo basi ni wazi unaweza kufikia utajiri mkubwa ambao upo mbele yako na unaokusubiri. Sasa bila kupoteza muda, naomba twende pamoja kwenye hatua muhimu ambazo unaweza ukazifuata kila siku na kila wakati hadi kuufikia  UTAJIRI. Tengeneza njia nyingi za kukuingizia kipato. Hakuna njia ya uhakika ambayo inaweza ikakufikisha kwenye utajiri kinyume na kuwa na vyanzo vingi vya pesa. Huwezi kufanikiwa kama ...

Njia 7 za kukuingizia hela hata kama umelala

Image
Karibu kila mtu katika nyakati fulani hufikiria biashara za kufanya au njia za kutengeza pesa ambazo zitamletea pesa hata wakati wa usiku akiwa amelala. Hii maana yake ni kwamba biashara huingiza pesa hata kama mmiliki wa hiyo biashara hatakuwepo pale. Biashara nyingi humlipa yule mwenye biashara kulinganna na masaa anayotumia kuitumikia biashara husika. Unaweza kuona sasa kwamba biashara ya namna hiyo haina tofauti kubwa na ajira ya kawaida. Kuna dhana iliyojengeka kwamba njia kubwa ya kuingiza pesa hata ukiwa umelala usiku wa manane ni kwa kupitia mtandao wa intaneti tu peke yake/biashara za mtandaoni au wengine mara nyingi huiita, njia ya kutengeneza pesa kupitia blogu . Lakini kiuhalisia mtu unaweza ukatengeneza pesa hata ukiwa umelala kwa kupitia biashara yeyote ile ilimradi tu umetengeneza mfumo(system) imara utakaowezesha shughuli kufanyika hata kama haupo pale. Hebu fikiria mmiliki wa mgahawa mkubwa wenye wafanyakazi kila idara kuanzia meneja mpaka mfagiaji, ana haja ya ku...

Kilimo bora cha chainese

Image
Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania. Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali. Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni. Jotolidi; Chinese au  linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c. Unyevunyevu; chinese  ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji. Udongo; chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6 Namna ya kuandaa shamba. Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda. Uandaaji w...

Kua mjasiriamali kwa kufuga kuku wa asili

Image
Mwanza: Ujasiliamali ni moja ya hatua katika mapambano dhidi ya umasikini, lakini pia ili kuweza kuwa mjasiriamali, yanahitajika maarifa ya ziada, ikiwamo ubunifu katika kuboresha shughuli unazozifanya ili ziwe na tija. Kama unaamini kweli kuwa unataka kuanzisha biashara yako mwenyewe lakini hujapata wazo la biashara lililostahiki, pumzika kwanza, halafu baada ya wiki moja au zaidi anza tena kuangalia mawazo mengine ya biashara kupitia Makala hii. Leo hii nitawaelezea kuhusu biashara ya kufuga kuku wa kienyeji ambavyo inaweza kukukwamua kutoka kwenye umasikini kwa kuwawezesha watu kutengeneza ajira zao binafsi. Nilipomtembelea mfugaji mwenye mafanikio jijini hapa, Bazil Dotto Bazil, nyumbani kwake Mh’andu Jijini hapa, ambapo alinisimulia kilichomsukuma kuingia katika ujasiriamali wa kufuga kuku wa kienyeji. “Watu wengi katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Technolojia wamekuwa wakiathirika na magonjwa mbalimbali kutokana na ulaji mbaya wa vyakula vyenye madawa hususani Kuku wa ku...

Mtaji wa kuku na mchanganuo wake mpaka unafanikiwa kwenye kuku wa kienyeji

Image
Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo. Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasa kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4. Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 – (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700. Ndugu mfuatiliaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka...

Formula 6 za ufugaji bora wa kuku

Image
   Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu: Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu, na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja SHs 10,000 mpaka 15,000, kuku wakubwa wanaanzia SHs 15,000 mpaka 30,000). Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi, kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote. Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio: 1. Aina ya kuku:  Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai. Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magon...

Siri iliojificha kwenye biashara za mitandao

Image
Biashara ya mtandao – hii ni biashara tofauti na watu kama Facebook, Zoom, matangazo ya kulipia au tovuti na barua pepe. Biashara hii au mfumo huu ambao unaitwa ujasiriamali, mara nyingi si halisi kama watu wanavyouuza mtaani. Watu wengi wameingia kwenye biashara hii kwa ushawishi mkubwa na wakiahidiwa pesa chap chap mara tu baada ya kujiunga. Hawa ni watu wajanja tu wa hapa mjini ambao wamekuwa wakileta mawazo ambayo hayana mantiki kibiashara hivyo wajinga ndio waliwao, ukweli mgumu kuumeza. Hapa tunaongelea maisha na taaluma,kuna kitu ukikijua kuhusu biashara ya namna hii inahusisha matapeli wakimataifa wakiwalenga watu wenye kutaka mafanikio ya chap chap hivyo kuwaingiza mjini kwa kiswahili cha bongo. Watu wengi wameingia bila kujua mtandao maana yake ni nini?  Mtandao kwa lugha za kigeni ni (network), biashara ya mtandao ninayoizungumzia hapa ambao unatakiwa kujua siri yake na utata wake ni Network Marketing. Huu mfumo ulikuwa na kutengeneza msululu wa watu ambao unawe...

Siri tano za mafanikio bila kua tegemezi

Image
Kila binadamu ameumbwa na kiu ya kufanikiwa katika kila kitu anachofanya. Mafanikio ndio kilele cha mlima mkubwa wa maisha ambao umejengwa kwa misingi na ngazi za mihangaiko na mitihani ambayo unapaswa kuivuka ili upumzike kwenye kilele hicho. Kwa bahati mbaya, unaposema ‘mafanikio’ wengi hufikiria kuhusu ‘utajiri’. Lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kati ya kuwa tajiri na kufanikiwa kiuchumi. Unaweza kuwa tajiri lakini ukawa bado hujafanikiwa. Kwa kuwa watu wanawaza utajiri kuwa ndio kigezo cha mafanikio hujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ajabu kwa lengo la kujizolea mali lakini mwisho huwa wanagundua kuwa hawajafanikiwa japo jamii inahisi wamefanikiwa. Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind). Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na ukosefu wa amani ya moyo. Hivyo, mafanikio ya njia ya mkato...